Matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye mfumo wa utoaji haki. Nini faida kwa wadau wa mahakama na mfumo mzima wa sheria.

Kiswahili ni Lugha ya Taifa na Matumizi ya Kiswahili yanazidi kukua kadri siku zinavyozidi kwenda, pamoja na kukua kwa lugha hii, Kiswahili kimekuwa hakitumiki katika mfumo mzima wa utoaji haki, kwa maana ya kwamba sheria zote za nchi yetu bado zipo kwa lugha ya Kiingereza na hata Mahakama zetu kuanzia ngazi ya Mahakama ya wilaya mpaka Mahakama ya rufani, lugha inayotumika ni Kiingereza. Kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kwenye shughuli mbali mbali za utoaji haki.

Lugha ya Kiswahili nchini imekuwa ikitumika kwenye mabaraza yote na Mahakama zote za Mwanzo tangu mwaka 1985 kwenye kuendesha mashauri na kutunza kumbukumbu zote, lakini kwenye mahakama za wilaya mpaka mahakama ya rufani, lugha ya kiswahili imekuwa ikutumika kuendesha mashauri laikini kumbukumbu zote za mahakama zimekuwa zikiandikwa kwa Kiingereza.

Serikali kupitia Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, wamepetisha mswada wa mabadiliko ya sheria (Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill of 2021 (Muswada), kupendekeza sheria zote za Tanzania Bara kuwa kwa Lugha ya Kiswahili; Hivyo basi katika kipindi hiki tunajadili kiundani ni nini dhumuni kuu la Serikali katika kuleta mapendekezo haya na ni nini zitakuwa changamoto za mabadiliko hayo, kama wanasheria na maafisa wa mahakama ni nini kingine cha ziada kinaweza kufanyika katika kuhakikisha lugha hii yetu adhimu inakuwa na kuendelea kutumika.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ads

ad